Bahá'í Prayers

Kiswahili : BARAZA LA KIROHO

Permanent Link

 

*Wakati wowote muingiapo chumba cha mashauriano semeni sala hii kwa moyo upumao na mapenzi ya Mungu na ulimi uliotakasika kutokana na vyote ila kumbukumbu Yake, ili kwamba Mwenye-uwezo wote aweze kwa neema kuwasaidia kupata ushindi mkuu:

Ee Mungu, Mungu wangu! Sisi tu watumishi Wako ambao wameugeukia kwa moyo uso Wako mtakatifu, ambao wamejitenga wenyewe kutokana na vyote kando Yako katika Siku hii tukufu. Tumekusanyika katika Baraza hili la Kiroho, tukiunganika katika maoni na mawazo yetu, na malengo yetu yakioanishwa kulitukuza Neno Lako kati ya wanadamu. Ee Bwana, Mungu wetu! Tufanye ishara za uongozi Wako mtakatifu, bendera za Imani Yako iliyotukuka kati ya watu, watumishi kwenye Ahadi Yako kuu, Ewe Bwana wetu Uliye Juu kabisa, wadhihirishaji wa Umoja Wako Mtakatifu katika Ufalme Wako wa Abha, na nyota angavu ziangazazo juu ya sehemu zote. Bwana! Tusaidie kuwa bahari zisukasukazo kwa mawimbi ya neema Yako ya ajabu, mito itiririkayo kutoka vilele Vyako vilivyotukuka kabisa, matunda mema juu ya mti wa Imani Yako ya mbinguni, miti ipepeayo kwa pepo za Baraka Yako katika shamba Lako la mizabibu la mbinguni. Ee Mungu! Zifanye roho zetu zitegemee Aya za Umoja Wako Mtakatifu, mioyo yetu ikichangamshwa na mmiminiko wa neema Yako, ili tuweze kuunganika hata kama mawimbi ya bahari moja na kuunganishwa pamoja kama miale ya nuru Yako ing’aayo; ili mawazo yetu, maoni yetu, yaweze kuwa kama uhalisia mmoja ukidhihirisha roho ya umoja ulimwenguni mwote. Wewe ni Mwenye neema, Karimu, Mpaji, Mweza yote, Mwenye rehema, Mwenye huruma.

 

Windows / Mac