Return   Facebook   Zip File

Arabic

1

EWE MWANA WA ROHO!

Shauri langu la kwanza ni hili: Uwe na moyo safi, mwema na ung’aao (mkunjufu) ili yako iwe enzi ya kale, isiyopoteana inayodumumilele.

2

EWE MWANA WA ROHO!

Kipenzi kabisa kuliko vitu vyote mbele ya macho Yaungu ni Haki; usiikwepe haki ikiwa unanihitaji Mimi, na wala usiipuze, ili Mimi nipate kukufanya msiri Wangu. Kwa msaada wake utapata kuona kwa macho yako mwenyewe na siyo kwa macho yaw engine, na utapata kujua kwa akili yako mwenyewe na siyo kwa akili ya jirani yako. Waza hili moyoni mwako; jinsi inavyokupasa uwe. Hakika haki ni zawadi Yangu kwako na ishara ya wema Wangu wa upendo. Basi iweke mbele ya macho yako.

3

EWE MWANA WA MTU!

Nikisetirika katika nafsi Yangu ya zama zisizokumbukwa na katika umilele wa kale wa asili Yangu, nijijua upendo Wangu kwako; ndipo nikakuumba wewe na kuichonga sanamu Yangu juu yako na kuudhihirisha uzuri Wangu kwako.

4

EWE MWANA WA MTU!

Nilipendezwa na kuumbwa kwako na ndipo nikakuumba. Kwa hiyo nipendi ili niweze kulitaja jina lako na kuijaza roho yako kwa pumzi ya uzima.

5

EWE MWANA WA KUWA!

Nipende ili Nami nipate kukupenda. Kama hunipendi, upendo Wangu hauwezi kukufikia pia. Elewa hili, Ewe mtumishi.

6

EWE MWANA WA KUWA!

Paradiso yako ni upendo Wangu, makao yako ya mbingu muungano tena Nami. Ingia humo na wala usingojee. Hili ndilo lililoamriwa kwa ajili yako katika ufalme Wetu ulio juu na milki Yetu inayotukua.

7

EWE MWANA WA MTU!

Ikiwa wanipenda, basi jikane (ipe kisogo nafsi yako) mwenyewe; na kama unaitafuta furaha yangu, isahau ya kwako; ili uweze kufa katika Mimi Name niweza kuishi ndani mwako milele.

8

EWE MWANA WA ROHO!

Hakuna amani yoyote kwako ila tu kwa kujikana mwenyewe na kunigeukia Mimi; kwani yakupasa kujitukuza katika jina Langu na siyo katika jina lako mwenyewe; kuweka imani yako ndani Mwangu na siyo mwako mwenyewe kwa maan nataka kupendwa pekee na juu ya vitu vyote vilipo.

9

EWE MWANA WA KUWA!

Upendo Wanju ndiyo ngome Yangu; anayeingia humo atasetirika na anayeipa kisogo (anayeikimbia) hakika atapotea na kuangamia.

10

EWE MWANA WA NENO!

Wewe ni ngome Yangu; ingia humo ili ukaw katika usalama. Jua kuwa upendo wangu u ndani yako ili upate kuniona kuwa niko karibu yako.

11

EWE MWANA WA KUWA!

Wewe ni taa Yangu na nuru Yangu iko ndani yako. Pata mng’ao wako kwayo na nitafute Mimi tu. Kwa maana nimekuumba tajiri na kukupa mbaraka Wangu kwa wingi.

12

EWE MWANA WA KUWA!

Kwa mikono yenye uwezo nilikufanya na kukuumba kwa vidole vyenye nguvu; na ndani yako nimeweka kiini cha nuru Yangu. Ridhika nayo na usitafute kingine chochote, kwa maana kazi Yangu imekamilika na amri Yangu yabidi. Usiipeleleze na wala usiwe na mashaka nayo.

13

EWE MWANA WA ROHO!

Nilikuumba tajiri; kwa nini unajishusha kwenye umaskini? Nilikuumba bora, kwa nini unajishusha? Kuktoka katika kiini cha maarifa nilikupa uhai, kwa nini unatafuta elimu kutoka mwingine kango Yangu? Kutoka katika udongo wa upendo nilikuumba, kwa jinsi gani unajishughulisha na mwingine? Geuza macho yako kwako mwenyewe, iliuweze kuniona nikisimama ndani yako, mwenye nguvu, mwenye uwezo na aliyepomwenyewe.

14

EWE MWANA WA MTU!

Wewe ni ufalme Wangu na ufalme Wangu hauangamii, kwa nini basi unaogopa kuangamia kwako? Wewe ni nuru Yangu na nuru Yangu haizimiki kamwe, kwa nin basi unaogopa kuzimika? Wewe ni utukufu Wangu na utukufu Wangu haufifi: wewe ni vazi Langu na vazi Langu halichakai kamwe. Dumu basi katika upendo wako kwangu ili uweze kuniona katika milki ya utukufu.

15

EWE MWANA WA NENO!

Geuza uso wako kuelekea uso Wangu na kuwakana wengine wote ila Mimi, kwa maana enzi Yangu hudumu na ufalme Wangu haupotei kamwe. Ikiwa utajitafutia mwengine zaidi Yangu, naam, kama ukitafuta daima katika ulimwengu mzima, utafutaji wako utakuwa bure.

16

EWE MWANA WA NURU!

Sahau yote ila Mimi, na zungumza na roho Yangu. Hiki ndico kiini cha amri Yangu, kwa hiyo igeukie.

17

EWE MWANA WA MTU!

Ridhika Nami na usitafute msaidizi mwingine yoyote. Kwa maana hakuna yeyote anayewez kukutosheleza daima ila Mimi.

18

Usiniombe kile tusichopendelea kwa ajili yako, hivyo ridhika na kile tulichoamuru kwa ajili yako, kwa maana hicho ndicho kinachokufaa kama utajiridisha nacho.

19

EWE MWANA WA KUONA KWA AJABU!

Nimepulizia ndani yako pumzi ya Roho Wangu ili uwe mpenzi Wangu. Kwa nini umeniacha na kujitafutia mpenzi mwingine isipokuwa Mimi?

20

EWE MWANA WA ROHO!

Dai Langu juu yako ni kubwa na haliwezi kusahaulika. Neema Yangu kwako ni tele na kaiwezi kufishwa. Upendo Wangu umejifanyia makao yake mwako na kauwezi kufichwa. Nuru Yangu imedhihirika kwako na haiwezi kutiwa giza.

21

EWE MWANA WA MTU!

Katika mti wa nuru ya utukufu nimekutundikia matunda bora sana. Kwa nini basi umegeukia mbali na kuridhika na kile kilicho duni? Kirudie basi kile kilicho bora zaidi kwa ajili yako katika ufalme wa mbinguni.

22

EWE MWANA WA ROHO!

Nimekuumba bora, lakini umejidhilisha mwenyewe. Basi inukia kile ambacho kwa ajili yake uliumbwa.

23

EWE MWANA WA MWENYE ENZI!

Nakuitia kwenye yale ya milele lakini wewe unatafuta kile kinachotoweka. Nini kilichokufanya kugeuka kutoka mapenzi Yetu na kutafuta yako?

24

EWE MWANA WA MTU!

Usiruke mipaka yako wala kudai yale usiyostahili. Sujudu mbele ya uso wa Mungu wako, Bwana mwenye nguvu na uwezo.

25

Usijivune juu ya maskini, kwa maana namwongoza katika njia yake na nakuona katika hali yako ya uovu na kukufadhaisha milele.

26

EWE MWANA WA KUWA!

Ungewezaje kuyasahau makosa yako mwenyewe na kujishughulisha na makosa ya wengine? Yeyote atendaye hivi amelaaniwa Nami.

27

EWE MWANA WA MTU?

Usinong’one dhambi za wengine iwapo wewe mwenyewe ni mtenda dhambi. Kama ukiivunja sharia hii utakuwa umelaaniwa, na kwa jambo hili Mimi nashuhudia.

28

EWE MWANA WA ROHO!

Fahamu kwa ukweli: Yule awaambiae watu wawe wa haki nay eye mwenyewe akatenda udhalimu huyo siye Wangu, hata akiitwa kwa jina Langu.

29

EWE MWANA WA KUWA!

Usiitakie roho yeyote kile ambacho wewe usingejitakia, na usitamke lile usilolitenda, Hii ndiyo amri Yangu kwako, ishike.

30

EWE MWANA WA MTU!

Usimnyime mtumishi Wangu anapotaka kitu chochote kutoka kwako, kwa maana uso wake ni uso Wangu; kwa hiyo tahayari mbele Yangu.

31

EWE MWANA WA KUWA!

Jifanyie hesabu mwenyewe kila siku kabla hujaitwa kwenye kutoa hesabu; kwa maana kifo, bila onyo, kitakufikia na utaitwa kutoa hesabu ya matendo yako.

32

EWE MWANA WA MWENYENZI!

Nimekifany kifo kuwa mjumbe wa kukuletea furaha. Kwa nini basi unasikitika? Niliiumba nuru ili ikuangazie utukufu wake juu yako.

Kwa nini unajificha kutoka kwake?

33

Kwa habari njema ya nuru nakusalimu: furahia! Kwenye baraza la utakatifu nakuita; udumu humo ili uweze huishi kwa amani milele.

34

EWE MWANA WA ROHO!

Roho ya utakatifu inakuletea habari za furaha za mwungano; kwa nini basi unasikitika? Roho ya uwezo inakuthibitisha katika hoja Yake, kwa nini unajificha? Nuru ya sura Yake inakuongoza; unawezaje kupotea?

35

EWE MWANA WA MTU!

Usisikitike ila tu iwapo uko mbali Nasi. Usifurahie ila tu iwapo unakaribia na kurudi Kwetu.

36

EWE MWANA WA MTU!

Shangilia katika furaha ya moyo wako ili uweze kustahili kukutana Nami na, kama kioo, kuonyesha uzuri Wangu.

37

EWE MWANA WA MTU!

Usijivue vazi Langu zuri na wala usiipoteze sehemu yako katika chemchemi Yangu ya ajabu, ili usije ukaona kiu milele.

38

EWE MWANA WA KUWA!

Tembea katika sharia Zangu kwa ajili ya upendo Wangu na jnyime kile unachokipenda kama unatafuta ridhaa Yangu.

39

EWE MWANA WA MTU!

Usiache amri Zangu kama unapenda uzuri Wangu, na usisahau mawaidha (mauidha) Yangu kama unataka kupata ridhaa Yangu njema.

40

EWE MWANA WA MTU!

Ungekwenda kwa kasi katika eneo kuu la anga na kupitia mapana ya mbingu, hata hivyo usingepata raha isipokuwa katika kutii amri Yetu na kunyenyekea mbele ya Uso Wetu.

41

EWE MWANA WA MTU!

Itukuze hoja Yangu li niweze kuzidhihirisha kwako siri za ukuu Wangu na kung’aa juu yako nuru ya milee.

42

EWE MWANA WA MTU!

Jinyenyekeze mbele Yangu ili kwa hisani nipate kukutembelea. Inuka kwa ajili ya ushindi wa hoja Yangu ili bado ungali duniani uweze kupata ushindi.

43

EWE MWANA WA KUWA!

Nitaje Mimi katika dunia Yangu ili niweze kukukumbuka katika mbingu Yangu. Ndipo macho Yangu na yako yatakapopata faraja.

44

EWE MWANA WA KITI CHA UTUKUFU!

Kusikia kwako ni Kusikia kwangu, kwa vivyo hivyo usikie. Kuona kwako ni kuona Kwangu, kwa vivyo hivyo uone, ili katika kiini cha ndani kabisa cha moyo wako uweze kushuhudia juu ya utakatifu Wangu ulio tukuka, Nami ndani ya nafsi Yangu Menyewe niwezekuhuhudia juu ya daraja tukufu kwa ajili yako.

45

EWE MWANA WA KUWA!

Tafuta kifo cha mfia dini katika nji aYangu; ridhika na furaha Yangu; na shukuru kwa kile nilichoamuru, ili upate pumzika Nami chini ya kivuli cha enzi nyuma ya hema la utukufu.

46

EWE MWANA WA MTU!

Fikiri na kuwaza. Je, ni nia yako kufia kitandani mwako, au kumwaga damu ya maiha yako mavumbini, mfia dini katika njia Yangu na hivyo kuwa udhihirisho wa amri Yangu na mfunuaji wa nuru Yangu katika paradise ya juu kabisa? Amua ipasavyo Ee mtumishi!

47

EWE MWANA WA MTU!

Kwa uzuri Wangu! Kuzipaka nywele zako kwa damu yako ni endo kubwa machoni pangu kuliko kuumbwa kwa ulimwengu na mwanga wa dunia zote mbili. Basi fanya juhudi kulipata hilo, Ee mtumishi!

48

EWE MWANA WA MTU!

Kwa kila kitu kuna ishara. Ishara ya upendo ni uvumilivu katika amri Yangu na subira katika majaribu Yangu.

49

EWE MWANA WA MTU!

Mpenzi wa kweli hutamani sana mateso kama vile mwasi atamanivyo msamaha na mtenda dhambi atamanivyo huruma.

50

EWE MWANA WA MTU!

Kama taabu itakupata sio katika njia Yangu, utawezaje kupita katika njia za walioridhika na furaha Yangu? Kama majaribu yatakusumbua siyo katika shauku yako ya kukutana Nami, utaezaje kuipata nuru katika upendo wako wauzuri Wangu?

51

Maafa Yangu ni majaliwa Yangu, kwa nje ni moto na kisasi, lakini kwa ndani ni nuru na rehema. Harakia kwake ili upate kuwa nuru ya milele na roho ya milele. Hii ndiyo amri Yangu kwako, uishike.

52

EWE MWANA WA MTU!

Kama neema itakuangukia, usifurahie, na kama udhilifu ukikujia, usisikitike, kwani vyote vitapita na vitakwisha.

53

EWE MWANA WA KUWA!

Kama umaskini utakufikia, usihuzunike moyoni; kwa maana kuna wakati Bwana wa neema (utajiri) atakutembelea. Usiogope udhilifu,kwa maana ukukufu iku moja utakaa juu yako.

54

EWE MWANA WA KUWA!

Kama moyo wako utauelekeza kwenye ufalme huu wa milele na usiopotea na uhai huu wa kale na udumuo daima, basi uache ufalme huu wa mauti na unaopita.

55

EWE MWANA WA KUWA!

Usijihughulishe na ulimwengu huu kwa maana kwa moo twaijaribu (twaipima) dhahabu na kwa khahabu twawajaribu (twawapima) watumishi Wetu.

56

EWE MWANA WA MTU!

Unataka dhahabu, lakini Mimi nataka uwe huru nayo. Unajidhania tajiri ukiwa nayo, lakini natambua utajiri wako katika kujitakasa nayo. Kwa uhai Wangu! Hii ndiyo hekima Yangu na hilo ni wazo lako, njia Yangu itapatanaje na yako?

57

EWE MWANA WA MTU!

Wape utajiri Wangu maskini Wangu ili mbinguni upokee kutoka katika ghala za uangavu usiofifia na hazina za utukufu wa milele. Lakini kwa uhai Wangu! Kuitoa roho yako ni jambo la fahari zaidi, kama ungeweza kuona kwa jicho Langu.

58

Helalu la uhai ni kiti Changu cha enzi; litakae na vitu vyote ili niweze kufanya makao Yangu humo na niweze kuishi humo.

59

EWE MWANA WA KUWA!

Moyo wako ni makao Yangu; utakase kwa mshuko Wangu. Roho yako ndio mahali pangu Pa ufunuo; isafishe kwa ajili ya udhihirisho Wangu.

60

EWE MWANA WA MTU!

Tia mkono wako kifunani Mwangu ili nipate kuinuka juu yako, mweupe na ang’araye.

61

EWE MWANA WA MTU!

Paa hadi mbingu Yangu ili uipate furaha ya mwungano, na kunywa mvinyo usio kifani kutoka katika kikombe cha utukufu wa kale na kale.

62

Siku nyingi zimepita juu yako ukiwa unajishughulisha na mawazo yako na fikara za upuzi. Kwa muda gani utaendelea kusinzia hatika kitanda chako? Inua kichwa chako toka usingizini, kwa maana jua limechomoza na kupanda hadi hichwani, huenda likakuangazia nuru ya uzui.

63

EWE MWANA WA MTU!

Mwangaza umekuangazia toka katika upeo wa Mlima mtakatifu na roho ya busara imepulizia pumzi katika Sinai ya moyo wako. Kwa hiyo jikomboe kutoka katika pazia la fikara zako duni na kuingia katika baraza Langu ili uweze kufaa kwa maiha ya milele na kushtahili kukutana Nami. Hivyo kifo kisipate kukujia, wala uchovu au maudhi.

64

EWE MWANA WA MTU!

Umilele Wangu ni ulimwengu (viumbe vyote) Wangu, nimeuumba kwa ajili yako. Ufanye kuwa vazi la hekalu lako Umoja Wangu ni kazi ya mikono Yangu; Nimeifanya kwa ajili yako; Jivike vazi hilo ili daima uwe ununuo wa uhai (nafsi) Wangu wa milele.

65

Utukufu Wangu ni zawadi Yangu kwako, na fahari Yangu isharaya reheme Yangu kwako. Lile linalonistahili hakuna yeyote atakayelielewa wala hakuna yeyote awezaye kulieleza. Hakiki nimelihifadhi katika ghala Zangu zilizofichwa na katika hazina za amri Yangu, kama ishara ya wema Wangu wa upendo kwa watumishi Wangu na huruma Yangu kwa watu Wangu.

66

ENYI WANA WA NAFSI TAKATIFU NA ISIYOONEKANA!

Mtazuiwa kunipenda Mimi na roho zitafadhaika wakati zinitajapo. Kwa maana akili haziwezi kunifahamu Mimi wala mioyo kunichukua Mimi.

67

EWE MWANA WA UZURI!

Kwa roho Yangu na kwa fadhili Yangu! Kwa rehema Yangu na kwa uzuri Wangu! Yote hayo niliyokufunulia kwa ulimi wenye uwenzo na kukuandikia kwa kalamu yenye nguvu yamelingana na uwezo wako na kuelewa kwako, siyo na hali Yangu wala mtumbuizo wa sauti Yangu.

68

ENYI WANADAMU!

Hamjui kwa nini tuliwaumba ninyi wote kutokana na mavumbi yale yale? Ili asiweko yeyote wa kujitukuza juu ya mwingine. Fikirini wakati wote mioyoni mwenu jinsi mlivyoumbwa. Kwa kuwa tumewaumba ainyi nyote kutokana na kitu kile kile kimoja mnapaswa kuwa hata kama roho moja, kutembelea miguu ile ile, kula kwa mdomo ule ule na kuishi katika nchi moja, ili kutoka katika nafsi yenu ya ndani kabisa, kwa vitendo vyenu na kazi zenu, ishara za umoja wenu na kiini cha kujitenga vipate kudhihirika. Hili ndilo shauri Langu kwenu, Enyi jeshi la mwangaza! Lisikieni shauri hili ili muweze kulipata tunda la utakatifu kutoka katika mti wa utukufu wa ajabu.

69

ENYI WANA WA ROHO!

Ninyi ni ghala ya kazina Yangu, kwa maana ndani yenu nimetunza lulu za siri Zangu na vito vya elimu Yangu. Vilinde kutokana na wageni kati ya watumishi Wangu na wasio wacha Mungu kati ya watu Wangu.

70

EWE MWANA WA YEYE ALIYESIMAMA PEKEE KWA UHALISI WAKE KATIKA UFALME WA NAFSI YAKE!

Jua kuwa nimepeperusha kwako manukato yote ya utakatifu, nimekufunulia kwa ukamilifu neno Langu, nimeikamilisha kupitia kwako Baraka Yangu na nimekutakia yaale niliyojitakia Mimi mwenyewe. Ridhika basin a furaha Yangu na uwe mwenye shukrani Kwangu.

71

EWE MWANA WA MTU!

Yaandike yote yale niliyokufunulia kwa wino wa nuru katika ubao wa roho yako. Kama hili halimo katika uwezo wako (basi fanya wino wako kiini cha moyo wako) Kama kuwezi kufanya hivyo basi andika kwa ule wino mwekundu uliomwangwa katika njia Yangu. Hili kweli ndilo tamu zaidi Kwangu kuliko vingine vyote, ili nuru yake idumu milele.

Persian

1

ENYI WATU WENYE AKILI YA KUJULIA NA MASIKIO YA KUSIKILIZIA!

Mwito wa kwanza wa Mpendwa ni huu: Ee ndege mwimbaji (nightingale) wa siri! Usiishi popote ila katika bustani ya miwaridi ya roho. Ewe mjumbe wa Solomon wa mapenzi! Usitafute kimbilio lolote ila katika Sheba ya mpendwa kabisa, na Ewe ndege (phoenix) asiyekufa! Usiishi popote ila katika kilima cha uaminifu. Humo ndimo makao yako yalimo, kama kwa mabawa ya roho yako utapaa mpaka mwenye milki isiyo kikomo na unatafuta kulifikia kusudi lako.

2

EWE MWANA WA ROHO!

Ndege hutafuta kiota chake; ndege mwimbaji uzuri wa waridi; huku ndege hao, mioyo ya wanadamu, ikiridhika na vumbi lipitalo, wampeita mbali yak iota chao cha milele, na kwa macho yaliyogeuziwa kwenye bwana la uzembe wamepotewa na utukufu wa uso mtakatifu. Ole! Jinsi gani inavyostaajabisha na kuhuzunisha; kwa kikombe kimoja tu kilichojaa, wamegeukia mbali na bahari zisukasukazo za Aliye Juu Kabisa na kuakia mbali na upeo ung’ano kabisa.

3

EWE RAFIKI!

Katika bustani ya moyo wako usipande kingine ila miwaridi ya upendo, na shauku usiuachilie mkono wako. Thamini urafiki wa wenye haki na uepukane na ushirikiano wowote na waovu.

4

EWE MWANA WA HAKI!

Mpenzi anaweza kwenda wapi kama si katika nchi ya mpendwa wake? Na ni mtafutaji gani apataye pumziko mbali na haja ya moyo wake? Kwa mpenzi wa kweli, mwungano ni uhai na utengano ni kifo. Kifua chake hakina saburi na moyo wake hauna utulivu. Maisha mengi sana angeyaacha kuharakia mwenye makao ya mpendwa wake.

5

EWE MWANA WA VUMBI!

Hakika nakuambia: Mzembe kabisa wa watu wote ni Yule ambaye anayeishana bure na kutafuta kujiendeleza mbele juu ya ndugu yake. Sema, Ee ndugu! Acha vitendo, siyo maneno, view pambo lako.

6

EWE MWANA WA DUNIA!

Ujue kwa kweli, moyo ambao ndani yake mabaki kidogo kabisa ya wivu bado yangalimo hautafikia kamwe ufalme wangu wa milele, wala kupumua hewa ya harufu nzuri za utakatifu zitokazo kwenye ufalme Wangu mtakatifu.

7

EWE MWANA WA UPENDO!

Wewe uko hatua moja tu kutoka vilele vitukufu vya juu na kutoka mti wa upendo wa mbinguni. Hukua hatua moja na kwa ya pili jongelea ufalme wa daima na ingia hema la milele. Tega sikio basi kwa yalo ambayo yamefunuliwa na kalamu ya utukufu.

8

EWE MWANA WA UTUKUFU!

Uwe mwepesi katika njia ya utakatifu na ingia mbingu ya mazungumzo Nami. Utakase moyo wako kwa mng’ao war oho na kimbilia kwenye baraza la Aliye Juu Kabisa.

9

EWE KIVULI KIPITACHO!

Pita mbele zaidi ya daraja dhalili za mashaka na uinuke mpaka kwenye vilele vitukufu vya uhakika. Fungua jicho la ukweli, ili uweze kuona Uzuri usio na utaji na ushangae: Atukuzwe Bwana, mwumbaji bora kuliko wote!

10

EWE MWANA WA TAMAA!

Lisikilize hili: Jicho la kibinadamu halitatambua kamwe uzuri wa milele, wala moyo mfu kufurahia chochote ila ua lililonyauka. Kwa maana kitu hutafuta kile kifananacho nacho na kufurahia kuandamana na kile cha aina yake.

11

EWE MWANA WA VUMBI!

Yapofushe macho yako ili uweze kuuona uzuri Wangu; ziba masikio yako ili usikie sauti yangu nyororo; jimwage elimu yote ili utwae sehemu ya elimu Yangu; na jitakase kutoka utajiri ili upate sehemu ya kudumu kutoka bahari ya utajiri Wangu wa milele. Pofua macho yako, yaani kwa vitu vingine vyote isipokuwa uzuri Wangu; ziba masikio yako kwa vyote isipokuwa neon Langu; jimwage elimu yote isipokuwa elimu Yangu; ili kwa macho safi, moyo safi na sikio la makini uweze kuingia baraza la utakatifu Wangu.

12

EWE MWANADAMU MWENYE PEO MBILI!

Fumba jicho moja na kulifungua linguine. Fumba moja kwa dunia na yoteyaliyomo humo, na fungua linguine kwa uzuri uliotukuka wa Mpendwa.

13

ENYI WANANGU!

Nachelea kuwa kwa kunyimwa sauti nzuir ya hua wa mbinguni msije mkadidimia mlikokuwa kwenye vivuli vya upotevu na bila kuutanzama kamwe uzuri wa waridi mkarudia kwenye maji na udongo.

14

ENYI RAFIKI!

Msiutupe hata uzuri wa milele kwa ajili ya uzuri ambao hauna budi ufe, na msiweke shauku yenu katika dunia hii ya kufisha ya vumbi.

15

EWE MWANA WA ROHO!

Majira yatafika ambapo ndege mwinbaji wa utakatifu hatazifunua tena siri za ndani na ninyi nyote mtapotewa na sauti tamu ya mbinguni na sauti itokayo juu.

16

EWE KIINI CHA UZEMBE!

Maelfu ya lugha za siri hunenwa katika kauli oja, na maelfu ya siri zilizofichwahufunuliwa katika wimbo mmoja. Lakini, ole! Hakuna sikio lisikialo wala moyo unaoelewa!

17

ENYI MARAFIKI!

Milango ifungukayo kwenye Pasipomahali imekaa wazi na makao ya mpendwa yamepambwa kwa damu ya mpenzi lakini wote isipokuwa wachachetu wangali wameukosa mji huu wa mbinguni, na hata kati ya wachache hao, hakuna waliokutwa na moyo safi na roho iliyotakasika ila konzi ndogo kabisa.

18

ENYI WAKAAJI WA PARADISO YA JUU KABISA!

Watangazieni watoto wa uhakika kwamba katika falme takatifu, karibu na paradise ya mbinguni, bustani mpya imetokea, bustani ambayo inazungukwa na wazalia wa ufalme wa juu ny wakaaji waishio milele wa paradise tukufu. Jitahidini, basi ili mpate kufikia daraja hiyo, ili mfumbue siri za mapenzi kutoka katika maua yake yapeperushwayo na upepo na kujifunza siri ya hekima kamilifu na takatifu kutoka katika matunda yake ya milele. Yamefarijika macho ya hao waingiao na kuishi humo!

19

ENYI RAFIKI ZANGU!

Je, mmeisahau asubuhi ile halisis na angavu, wakati katika mazingira yale yaliyotukuka na yaliyobarikiwa mlipokusanywa mbele Yangu chini ya kivuli cha mti wa uzima ulipandwa katika paradise tukufu kabisa? Kwa hofu mlinisikiliza nikiyatamka maneno haya matatu matakatifu kuliko yote: Enyi rafiki! Msipendelee mapenzi yenu zaidi kuliko ya Kwangu, mistake kamwe kile ambacho sikuwatakieni, na msinikaribie kwa mioyo iliyokufa, iliyonajisiwa kwa tama na shauku za kidunia. Kama mngetakasa roho zenu tu saa hii hii mngekumbuka mahali pale na mazingara yale, na ukweli wa tamko Langu utadhihirika kwenu ninyi nyote.

20

Katika msitari wa nane wa mistari mitakatifu kabisa, katika Kibao cha tano cha Paradiso, Yeye asema:

ENYI MNAOLALA KAMA WAFU KATIKA KITANDA CHA UZEMBE!

Miaka imepita na maisha yenu ya thamani yanakaribia mwisho lakini hakuna hata pumzi moja ya utakaso iliyofikia baraza letu takatifu toka kwenu. Ingawa mmezama katika bahari ya mashaka na kutoamini, lakini kwa midomo yenu mnaikiri ile imani moja tu ya kweli ya Mungu. Yule nimchukiaye ninyi mmempenda, na kumfanya adui Yangu kuwa rafiki. Hata hivyo mnatembea katika dunia Yangu kwa raha na kuridhika wenyewe, bila kujali kuwa dunia yangu imechoshwa nanyi na kila kutu duniani kinawakataa na kuwakwepa. Kama mngeyafumbua tu macho yenu, hakika mngependelea zaidi maelfu ya misiba kuliko furaha hii na mngehesabu kifo chenyewe kuwa bora kulilko maisha haya.

21

EWE UMBILE LA VUMBI LIENDALO!

Natamani mazungumzo nawe lakini wewe huweki tumaini Kwangu. Upanga wa usasi wako umeuangusha mti wa tumaini lako. Kila wakati niko karibu nawe lakini wewe daima uko mbali Name. Niekuchagulia utukfu wa milele, lakini wewe umejichagulia aibu isiyo na mpaka. Rudi muda ungalip bado na usipoteze nafasi yako.

22

EWE MWANA WA TAMAA!

Kwa miaka mingi wenye elimu na wenye hekima wamejaribu na kushindwa kufikia mbele ya Mtukufu uliko wote; wameyatumai maisha yao katika kumtafuta Yeye, lakini hata hivyo hawakuuona uzuri wa sura Yake. Wewe bila juhudi yoyote umeifikia shabaha yako na bila kutafuta umepata makusudi ya kutafuta kwako. Lakini, hata hivyo umebakia umezongamezwa kabisa katika utando wa nafsi mpaka macho yako hayakuuona uzuri wa Mpendwa, wala mkono wako haukuugusa upindo wa vazi Lake. Ninyi mlio na macho mnatazama na kustaajabu.

23

ENYI MUISHIO KATIKA MJI WA MAPENZI!

Mivumo ya pepo za kifo imeuzingira mshumaa wa milele na uzuri wa Kijana wa mbinguni umefunikwa katika giza la vumbi. Mkubwa wa wafalme wa apenzi amefanyiwa uovu na watu wa dhuluma, na hua wa utakatifu amefungwa katika makucha ya mabundi. Wakaaji katika hema la fahari na jeshi la mbinguni hulia na kuomboleza wakati ninyi mnapumzika katika ufalme wa uzembe na kujidhania wenyewe kama marafiki wa kweli. Jinsi gani mawazo yenu yasivyofaa!

24

ENYI MLIO WAPUMBAVU, LAKINI MNATAJWA KUWA WENYE HEKIMA!

Kwa nini mnavaa mtindo wa wachungaji, wakati ndani mmekuwa mbwa mwitu, mkilidhamiria kundi langu? Mmekuwa kama nyota inayochomoza kabla ya mapambazuko na ambayo, japo yaonekana ing’aayo na itoayo mwanga kuwapotosha wasafiri wa mji Wangu katika njia za maangamizi.

25

ENYI MNAOONEKANA KUWA WASAFI NA KUMBE NDANI WACHAFU!

Mko kama maji safi lakini machungu, ambayo kwa kutazamwa kwa nje yanaonekana safi kabisa lakini ambayo yakipimwa na Mpimaji mtakatifu hakuna hata tone linalokubaliwa. Naam, mwonzi wa jua huangukia sawasawa juu ya vumbi na juu ya kioo, lakini hutofautiana katika kurudisha nuru hata kama nyota inavyotofautiana na dunia: hapana, tofauti yenyewe haipimiki!

26

EWE RAFIKI YANGU KWA MANENO!

Fikiri kwa muda kidogo. Umepata kusikia hata kidogo kwamba rafiki na adui waishi katika moyo mmoja? Basi mtupe nje mgeni ili Rafiki aingie nyumbani Kwake.

27

EWE MWANA WA VUMBI!

Yote yaliyo mbinguni na duniani nimeamuru kwa ajili yako, isipokuwa moyo wa mtu ambao nimeufanya makao ya uzuri na utukufu Wangu; lakini umempa nyumba Yangu na makao yangu mwingine zaidi Yangu; na wakati wowote udhihirisho wa utakatifu Wangu alipotafuta makao Yake, mgeni alimkuta hapo, na pasipo makao, alikimbilia mahali patakatifu pa Mpenzi. Hata hivyo nimeificha siri yako na sikutaka aibu yako.

28

EWE KIINI CHA TAMAA!

Katika mapambazuko mengi nimegeuka toka milki za Pasipomahali mpaka kwenye makao yako na kukukuta katika kitanda cha starehe ukijishughulisha na wengine zaidi Yangu. Hapo, kama mwonzi war oho, nilirudi kwenye milki za utukufu wa mbinguni na bila kulinong’ona jambo hilo katika makimbilio Yangu juu kwa majeshi ya utakatifu.

29

EWE MWANA WA UKARIMU!

Kutoka katika takataka sisizo kitu, kwa udongo wa amri Yangu nilikufanya utokee, jna nimeamuru kwa mafunzo yako kila chembe katika uhai na kiini cha viumbe vyote. Hivyo, kabla hujatoka tumboni mwa mama yako nimekuwekea chemchemi mbili za maziwa yang’aayo, macho ya kukuchunga na mioyo ya kukupenda. Kwa wema Wangu wa upendo, chini ya kivuli cha rehema Yangu nilikulea, na kukulinda kwa kiini cha neema na fadhili Yangu. Na kusudi Langu katika haya yote lilikuwa kwamba uweze kuupata ufalme Wangu wa milele na kustahili majaliwa Yangu yasiyoonekana. Na lakini wewe ulibake bila kusikia na ulipokuwa mtu mzima ulipuuza Baraka Zangu zote na kujishughulisha mwenyewe na fikara zako za upuzi, kiasi ambacho ulikuwa msahaulifu kabisa, na ukiipa kisogo milango ya Rafiki, ukaishi katika mabaraza ya adui Yangu.

30

EWE MTUMWA WA DUNIA!

Katika mapambazuko mengi upepo mwanana wa wema wa upendo Wangu umekupitia na kukukuta katika kitanda cha uzeme ukiwa umelala fofofo. Ukiomboleza basi hali yako, ulirudi ulikotoka.

31

EWE MWANA WA DUNIA!

Kama ungalikuwa na Mimi; usimtafute yeyote zaidi Yangu; na kama ungeutazama uzuri Wangu fumba macho yako kwa dunia na yote yaliyomo ndani yake; kwa maana mapenzi Yangu na mapenzi ya mwingine zaidi Yangu, kama moto na maji, haviwezi kukaa pamoja katika moyo mmoja.

32

EWE MGENI ULIYEFANYWA RAFIKI!

Mshumaa wa moyo wako huwashwa kwa mkono wa uwezo Wangu , usiuzime kwapepo za upinzani za nafsi na shauku. Mponyaji wa maradhi yako yote ni kunikumbuka Mimi, usisahau jambo hilo. Ufanye upendo Wangu kuwa hazina yako na utunze kama macho yako yenyewe na uhai.

33

EWE NGUGU YANGU!

Yasikilize maneno ya kufurahisha ya ulimi Wangu uliotiwa asali na kunywa mkondo wa utakatifu usioelezeka kutoka katika midomo Yangu itoayo sukari. Panda mbegu za hekima Yangu takatifu katika udongo safi wa moyo wako na zimwagilie maji ya uhakika, ili maua (ya hyacinth) ya elimu na hekima Yangu yachipuke mabichi nay a kijani katika mji mtakatifu wa moyo wako.

34

ENYI WAKAAJI WA PARADISO YANGU!

Kwa mikono ya wema wa upendo nimepanda katikabustani takatifu ya paradise mti mchanga wa upendo wenu na urafiki na kuumwagilia kwa manyunyu mema ya neema Yangu ya kuruma; kwa vile sasa wakati wake wa kuzaa matunda umewadia, mjibidishe ili uweze kulindwa na usije ukateketezwa kwa mwali wa tama na shauku.

35

ENYI RAFIKI ZANGU!

Zimeni taa ya ukosefu na muwashe katika mioyo yenu kurunzi ya milele ya uongozi mtakatifu. Kwa maana si muda mrefu kupita wapimaji wa wandamu, machoni patakatifu pa Mwabudiwa, hawatakubali chochote ila tu wema mtupu na matendo ya utakatifu usio na mawaa.

36

EWE MWANA WA VUMBI!

Wenye hekima ni wale wasiosema mpaka wanaposikilizwa, kama mwenye kikombe ambaye hakitoi mpaka anapompata mtafutaji na kama mpenzi ambaye halii kutoka katika kina cha moyo wake mpaka anapoutazama uzuri wa mpendwa wake. Kwa hiyo panda mbegu za hekima na elimu ktika udongo safi wa moyo nakuzificha humo mpaka maua (ya hyacinth) ya hekima takatifu yachipuke toka moyoni na siyo kutoka katika matope na udongo.

Katika msitari wa mwanza wa Andiko imenakiliwa na kuandikwa, na katika patakatifu pa hema la Mungu imefichwa:

37

EWE MTUMISHI WANGU!

Usiuache ufalme wa milele kwa ajili ya kile kinachopotea na usiitupe enzi ya mbinguni kwa tama ya dunia. Huu ndio mto wa uhai wa milele ambao umetiririka kutoka katika chemchemi ya kalamu ya mwenye rehema; heri ni yao wale wanywao.

38

EWE MWANA WA ROHO!

Lipasulie mbali tundu lako, nahata kama ndege (phoenix) wa mapenzi paa katika mbingu ya utakatifu. Jikane mwenyewe na ukijazwa na roho ya huruma, kaa katika milki ya utakatifu wa mbinguni.

39

EWE MAZO WA VUMBI!

Usiridhike na starehe ya siku ipitayo na usijnyie mapumziko ya milele. Usiibadilishe bustani ya furaha ya milele kwa fungu la mavumbi ya dunia ya mauti. Amka kutoka katika gereza lako upae katika mashamba ya utukufu huko juu, na kutoka katika tundu lako la mauti ruka mpaka katika paradise ya Pasipo-Mahali.

40

EWE MTUMISHI WANGU!

Jifungue kutoka kwenye minyororo ya dunia hii na iachilie roho yako toka katika gereza la nafsi. Chukua nafasi yako, kwa maana haitakujia tena.

41

EWE MWANA WA KIJAKAZI WANGU!

Kama ungeiona enzi ya milele, ungejitahidi kupita kutoka katika dunia hii ipitayo upesi. Lakini kukuficha ile moja na kukufunulia nyingine ni siri ambayo hakuna ila tu aliyesafi moyoni aweza kufahamu.

42

EWE MTUMISHI WANGU!

Jisafishe moyo wako kutokana na uovu na, bila wivu, ingia katika baraza tukufu la utakatifu.

43

ENYI RAFIKI ZANGU!

Tembeeni katika njia za furaha njema ya Rafiki, na mjue kuwa furaha Yake imo katika furaha ya viumbe Wake. Yaani: hakuna mtu angeingia nyumbaya rafiki yake ila kwa radhi ya rafiki yake, wala kushika mali zake wala kupendelea nia yake mwenyewe zaidi kuliko ya rafiki yake na kwa jinsi yoyote asijitafutie manufaa juu yake. Lifikirini hili, ninyi mlio na mioyo ya kuona!

44

EWE MWENZI WA KITI CHANGU CHA UFALME!

Usisikie uovu, na usione uovu, usijishushe, wala kuhema kwa mashaka na kulia. Usiseme uovu, ili usiweze kuusikia ukisemwa kwako, na usiyakuze makosa yaw engine ili makosa yako mwenyewe yasije yakaonekana makubwa; na usimtakie fedheha yeyote, ili fedheha yako mwenyewe isifichuliwe. Ihi basi siku za uhai wako, ambazo ni chache kuliko muda mfupi upitao, ukiwa na akili yako isiyo na mawaa, moyo wako usio na uchafu, mawazo yako safi, na asili yako iliyo takasika ili kwamba, ukiwa huru na aliyeridhika, uweze kuliwekea mbali umbo hili la mauti, na kwenda kwenye paradise isiyoelezeka na kuishi katika ufalme wa milele hata milele.

45

OLE! OLE! ENYI WAPENZI WA TAMAA ZA DUNIA!

Kama wepesi wa radi mmempita Yule Mpendwa, na kuiweka mioyo yenu kwenye mawazo ya kishetani. Mnapiga magoti mbele ya mawazo yenu ya upuzi na kuyaita ukweli. Mnageuzia macho yenu kuelekea kwenye mwiba na kuuita ua. Hata pumzi safi hamjapumua, wala upepo wa kujitenga haujapeperushwa kutoka katika mashamba ya mioyo yenu. Mmeyatupa (achilia mbali) mwenye upepo mawaidha ya upendo ya. Mpendwa na kuyafuta kabisa kutoka katika ubao wa mioyo yenu, na kama wanyama wa mwituni, mnatembea na kuwa na uhai wenu katika malishoya tamaana shauku.

46

ENYE NDUNGU KATIKA NJIA!

Kwa nini mmeacha kumbukumbu (kumtaja) ya Yule Apendwaye na kuwa mbali na usoni Pake patakatifu? Kiini cha uzuri kiko ndani ya hema lisilo na kifani, kimewekwa katika kiti kitukufu cha ufalme, huku mkijishughulisha na mabishano ya kipuzi. Harufu tamu za utakatifu zinanukia pumzi ya na ukatimu inapeperushwa, lakini nyote mnateseka sana na kunyimwa hivyo. Ole wenu na wale ambao hutembea katika njia zenu na kufuata nyayo zenu!

47

ENYI WANA WA TAMAA!

Wekeeni mbali vazi la majivuno na mjivue vazi la ufidhuli.

48

Katika msitari wa tatu wa mistari takatifu kabisa, ikiaadikwa na kunakillwa juu ya Ubao wa kito chekundu cha thamani kwa kalamu ya kisichoonekana, hii imefunuliwa:

ENYI NDUGU!

Myumiliane mmoja kwa mwingine na msiiweke shauku yenu katika vitu vya chini. Msijivunie fahari yenu na wala msione aibu kwa udhilifu. Kwa uzuri Wangu! Nimeumba vitu vyote kutoka kwenye mavumbi, na mavumbini Mini nitavirudisha tena.

49

ENYI WANA WA VUMBI!

Waambieni matajiri kuhusu kuhema kwa mashaka kwa maskini usiku wa manana, ili ukaidi usije ukawaongoza kwenye njia ya maangamizi, na kuwakoesha Mti wa Utajiri. Kutoa na kuwa mkarimu ni sifa Zangu; heri ni yake Yule ajipambaye kwa njema Zangu!

50

EWE ASILI HALISI YA SHAUKU!

Wakea mbali tama na tafuta kuridhika; kwa maana mwenye tama daima amenyimwa, na mwenye kuridhika daima amependwa na kusifiwa.

51

EWE MWANA WA KIJAKAZI WANGU!

Usisumbuke katika umaskini wala kuwa mtumainifu katika utajiri, kwa maana umaskini hufuatwa na utajiri, na utajiri hufuatwa na umaskini. Lakini kuwa maskni katika yote isipokuwa Mungu ni karama ya ajabu; usipunguze thamani yake, kwa maana mwishowe itakufanya tajiri katika Mungu, na kwa jinsi hii utapata kufahamu maana ya msemo, “Kwa kweli ninyi ndio maskini,” na maneno matakatifu “Mungu ndiye mwenye vyote,” kama asubuhi ahlisi, yatapambazuka kwa uangavu wa utukufu katia upeo wa moyo wa mpenzi, na kukaa salama katika kiti ha enzi ya utajiri.

52

ENYI WANA WA UZEMBE NA SHAUKU!

Mmemruhusu adui Yangu kuingia nyumba Yangu na kumptupa nje rafiki Yangu, kwa maana mmetunza upendo wa mwingine zaidi Yangu katika mioyo yenu. Yasikilizeni maneno ya Rafiki na kuigeukia paradise Yake. Marafiki wa kidunia, wakijitafutia faida yao wenyewe, wanaonekana, kupendana, lakini Rafiki halisi amewapenda na kuwapenda kwa ajili yenu wenyewe; kwa kweli amepata mateso yasiyohesabika kwa ajili ya uongozi wenu. Msiwe wasio waaminifu kwa Rafiki kama huyo, la afadhali mkimbilie Kwake. Hivi ndivyo ilivyo nyota ya mchana ya neon la kweli na uaminifu, ambayo imepambazuka juu ya upeo wa kalamu ya Bwana wa majina yote. Fungueni masikio yenu ili mpate kulisikia neon la Mungu, Msaada katika mashaka, Aishiye Mwenyewe.

53

ENYI MNAOJIVUNIA UTAJIRI WA KIBINADAMU!

Jueni kwa kweli kuwa mali ni kipingamizi kikuu kati ya mtafutaji na haja yake, kati ya mpenzi na mpendwa wake. Matajiri isipokuwa wachache, kwa jinsi yoyote, hawatalifikia baraza la machoni Pake wala kuingia mji wa ridhaa na shukurani. Herini yake Yule basi, ambaye, akiwa ni tajiri, hazuiwi na utajiri wake kutoka kwenye ufalme wa milele, wala kunyimwa nao milki isiyopotea. Kwa Jina Kuu kuliko yote! Utukufu wa mtu tajiri kama huyo utawaangazia wakaaji wa mbinguni, kama vile jua linavyo waangazia watu wa dunia!

54

ENYI MATAJIRI DUNIANI!

Maskini kati yenu ni dhamana Yangu; itunzeni dhamana Yangu; na msidhamirie tu kwenye starehe yenu wenyewe.

55

EWE MWANA WA SHAUKU!

Jitakase kutokana na najisi ya utajiri na katika amani kamili jongelea milki ya umaskini; ili kutoka katika chemchemi ya kujitenga uweze kunywa mvinyo wa maisha ya milele.

56

EWE MWANAGU!

Mwandamano na watu waovu huongeza huzuni, huku urafiki na watu wenye haki huisafisha kutu kutoka moyoni. Yule atakaye kuzungumza na Mungu, mwache aende kwenye urafiki wa wapendwa Wake; na atakaye kulis kia neon la Mungu, acha ayape sikio maneno ya wateule Wake.

57

EWE MWANA WA VUMBI!

Tahadhari! Usitembee na muovu na usitafute urafiki naye, kwa maana urafiki wa namna hiyo huigeuza nuru va moyo kuwa moto wa jehanum.

58

EWE MWANA WA KIJAKAZI WANGU!

Ikiwa unatafuta neema ya Roho Mtakatifu, ingia katika urafiki na mwenye haki, kwa maana yeye amekunwa kikombe cha uzima wa milele kwenye mikono ya Mchukuzi kikombe aishiye milele na hata kama asubuhi halisi ahuisha na kuing azia mioyo ya wafu.

59

ENYI MSIOSIKIA!

Msifikirie kuwa siri za mioyo zimefichwa, hapana, jueni kwa uhakika kuwa katika herufi safi zimechongwa na kudhihirishwa wazi katika mbele ya Mtakatifu.

60

ENYI RAFIKI!

Hakima masema, chochote mlichoficha katika mioyo yenu kwetu Sisi kiko wazi na kudhihirika kama mchana; lakini kwamba kimefichwa ni kwa ajili ya rehema na fadhili Yetu na siyo kwa ajili ya kustahili kwenu.

61

EWE MWANA WA ADAMU!

Tone la umande kutoka katika bahari ya kina kisichopmika ya rehema Yangu nimewadondoshea watu wa dunia, lakini kukuta hakuna aliyeligeukia, kwa kuwa kila mmoja amegeukia mbali ya mvinyo wa mbnguni wa umoja na kugeukia mashinda machafu ya unajisi, na akiridhika na kikombe cha mauti, amekiwekea mbali kikombe cha uzuri wa milele. Kiovu kile alichoridhika nacho.

62

EWE MWANA WA VUMBI!

Usigeuze macho yako mbali kutoka mvinyo usio na kifani wa Mpendwa wa milele, na usiyafumbue kwenye mashinda machafu nay a mauti. Twaa kutoka mikononi mwa Mchukua-kikombe mtakatifu kikombe cha uzima wa milele ili hekima yote iwe yako na uweze kuisikia auti isiyoelezeka iitayo kutoka katika milki ya kusikoonekana. Lieni kwa sauti, enyi mlio na lengo dogo! Kwa nini mmegeukia mbali na mvinyo Wangu mtakatifu na wa milele na kugeukia kwenye maji yanyaukayo upesi?

63

ENYI WATU WA DUNIA!

Jueni kweli kuwa maafa yasiyotazamiwa yanawafuata na adhabu ya majonzi inawangojea. Msidhanie kuwa matendo mliyofanya yamefutwa kutoka mbele ya macho Yangu. Kwa uzuri Wangu! Matendo yenu yote yamechorwa na kalamu Yangu kwa herufi safi juu ya ibao vya kito cha kijani.

64

ENYI WAONEZI WA DUNIA!

Ondoeni mikono yenu kutoka kwenye udhalimu, kwa maana nimejifunga Mwenyewe kwa kiapo kutosamehe udhalimu wa mtu yeyote. Hili ndilo agano Langu nililoamuru bila kubadilika katika ubao (wa maandiko) uliohifadhiwa na kulifunga kwa muhuri wa utukufu Wangu.

65

ENYI WAASI!

Uvumilivu Wangu umewapa moyo na ustahimilivu Wangu umewafanya wazembe, kwa jinsi ambayo mmemchochea farasi mkali wa shauku katika njia za hatari zinazoongozea kwenye maangamizi. Je, mmenidhania kuwa sijali au kwamba sikujua?

66

ENYI WAHAMIAJI!

Ulimi nimeukusudia kwa kumbukumbu Yangu, msiunajisi kwa ukashifu. Kama moto wa nafsi ukiwashinda, kumbukeni makosa yenu wenyewe na siyo makosa ya viumbe Wangu, kwa kuwa kila mmoja wenu anaijua nafsi yake mwenyewe zaidi kuliko anavyowajua wengine.

67

ENYI WANA WA MAWAZO!

Jueni kwa uhakika kuwa wakati alfajiri ing’aayo ipambazukapo juu ya upeo wa utakatifu wa milele, siri za kishetani na matendo yaliyotendwa katika giza la usiku yatafichuliwa na kudhihirishwa mbele ya watu wa dunia.

68

EWE GUGU LICHIPUKALO TOKA MAVUMBINI!

Kwa nini mikono yako hii michafu haikuligusa kwanza vazi lako mwenyewe, na kwa nini ukiwa na moyo wako umechafuliwa na tama na shauku unataka kuzungumza Nami na kuingia milki Yangu takatifu? Mbali, uko mbali na kile unachokitaka.

69

ENYI WANA WA ADAMU!

Maneno matakatifu na matendo safi na mema hupaa hadi mbingu ya utukufu wa mbinguni. Jitahidini ili matendo yenu yatakaswe kutoka kwenye vumbi la nafsi na unafiki na kupata ridhaa (kukubaliwa) kutika baraza la utukufu; kwa maana si muda mrefu wapimaji wa wanadamu, mbele ya utakatifu wa Mwabudiwa, hawatakubali chochote ila tu wema kamili na matendo ya usafi usio na dosari. Hii ndiyo nyota ya mchana ya hekima na siri takatifu ambayo imeangaza juu ya upeo wa kusudi takatifu. Wamebarikiwa wao ambao wanaigeukia.

70

EWE MWANA ANASA ZA DUNIA!

Ni ya kupendeza milki ya kuwa (kuwa hai), kama ungeifikia; ni ya fahari milki ya umilele, kama utapita dunia ya mauti; ni tamu furaha kuu takatifu kama utakunywa katika kikombe kisichoeleeka kutoka katika mikono ya Kijana wa mbinguni. Kama utafikia daraja hili, utaokolewa kutoka katika maangamizi na kifo, kutoka katika taabu na dhambi.

71

ENYI RAFIKI ZANGU!

Kumbukeni ahadi ile ambayo mmeifanya Nami juu yaa Mlima Parani, ulioko ndani ya mipaka mitakatifu ya Zamani Nimeyachukua majeshi ya mbinguni na wakaaji katika mji wa uzima wa milele kushuhudia, lakini sasa simpati yeyote aliye mwaminifu katika ahadi hiyo; Kwa hakika kiburi na uasi vimeifutia mbali kutoka mioyoni kwa jinsi ambayo hakuna alama yake iliyobakia. Hata hivyo nikijua hili, nilingojea na sikultfichua.

72

EWE MTUMISHI WANGU!

Wewe u kama upanga uliyochovywa (fanywa mgmu) vizuri sana uliofich wa katikagiza la ala yake na thamani yake kufichwa kutoka katika maarifa ya fundi. Kwa hiyo toka nje kutoka katika ala ya nafsi na tama ili thamani yako ipate kufanywa kung’aa na kudhihirika duniani pote.

73

EWE RAFIKI YANGU!

Wewe u nyota ya mchana ya mbingu za utakatifu Wangu, usiache najisi ya dunia iushinde wangavu wako. Pasulia mbali utando wa ukaidi, ili kutoka nyuma ya mawingu uweze kutokea uking’aa na kuvivika vitu vyote vazi la uzima.

74

ENYI WANA WA MAJIVUNO!

Kwa ajili ya enzi ipitayo upesi mmeiacha milki Yangu ya milele, na mmejipamba wenyewe kwa mavazi ya urembo ya kujifurahisha ya dunia na kukifanya kitu cha kujivunia. Kwa uzuri Wangu! Wote nitawakusanya chini ya kile kifuniko cha rangi moja cha vumbi na kufutia mbali aina zote hizi za rangi mbali mbali isipokuwa hao waichaguao Yangu mwenyewe, na hiyo ni kujitakasa na kila rangi.

75

ENYI WANA WA UZUMBE!

Msiweke shauku zenu katika enzi ipitayo na msiifurahie. Ninyi ni kama ndege asiye na hadhari ambaye kwa imani kabisa huimba juu ya tawi; mpaka kwa ghafla Yule mwindaji Kifo humtupa juu ya mavumbi, na sauti tamu, umbo na rangi vinatoweka bila kuacha alama. Kwa hiyo angalieni, Enyi watumwa wa tamaa!

76

EWE MWANA WA KIJAKAZI WANGU!

Uongozi umekuwa daima ukitolewa kwa maneno, na sasa unatolewa kwa mateno. Kila mmoja lazima aonyeshe matendo yaliyo safi na matakatifu, kwa maana maneno ni mali ya wote sawasawa, lakini matendo kama haya ni (mali) ya wapendwa Wet utu. Jitahidini basi kwa moyo na roho kujipambanua wenyewe kwa matendo yenu. Kwa jinsi hii Sisi tunawashauri katika kibao (cha maandiko) hiki kitakatifu na king’aacho.

77

EWE MWANA HAKI!

Katika majira ya usiku uzuri wa Uhai wa milele umekwenda kutoka katika mlima wa zumaradi wa uaminifu mpaka kwenye Sadaratu’lMuntaha na kulia kwa maomboleo kwa jinsi ambayo kwamba majeshi ya mbinguni na wakaaji wa milki ilio juu waliomboleza kwa kulia Kwake. Ndipo iliulizwa Kwanini maombolezo na kilio? Yeye akajibu: Kama nilivyoamriwa, nilingojea kwa tumaini juu yam lima wa uaminifu, lakini sikuvutu manukato ya uaminifu kutoka kwa wao wakaao duniani. Basi milpoamriwa kurudi niliona, na lo! hua fulani wa utakatifu waliteswa sana katida makucha ya mbwa wa dunia. Ndipo Mwanamwali wa mbinguni aliharakia nje bila utaji na aking’aa kutoka katika jumba Lake lisiloelezeka, na akauliza majina yao, na yote yalitajwa isipokuwa moja. Na ilipo himizwa, herufi ya kwanza ya jina hilo ilitamkwa, ndipo wakaaji wa vyumba vya mbinguni walitoka kwa haraka nje ya makao yao ya utukufu. Na wakati herufi ya pili ilipotamkwa, walianguka chini mavumbini, wote kwa pamoja. Wakati huo sauti ilisikika kutoka ndani kabisa ya mahali patakatifu: “Mpaka hapo na siyo mbaii zaidi.” Kwa hakika tunakishuhudia kile ambachowamekitenda na sasa wanakitenda.

78

EWE MWANA WA KIJAKAZI WANGU!

Kunywa kutoka katika ulimi wa mwenye rehema mkondo wa siri takatifu, na kutazama kutoka katika mapambazuko ya meneno matakatifu fahari iliyofunuliwa ya nyota ya mchana ya hekima. Panda mbegu za hekima Yangu takatifu katika udongo safi wa moyo na uzinyweshe kwa maji ya uhakika, ili maua (ya hyacinth) ya elimu na hekima yaweze kuchipuka mabichi nay a kijani kutoka katika mji mtakatifu wa moyo.

79

EWE MWANA WA TAMAA!

Kwa muda gani utaendelea kupaa katika milki za tama? Mabawa nimekupa ili uweze kupaa mpaka kwenye milki za utakatifu usioelezeka na siyo kwenye nchi za fikara za kishetani. Chanuo pia nimekupa ili uweze kuzichanua nywele Zangu nyeusi na siyo kuliparura koo Langu.

80

ENYI WATUMISHI WANGU!

Ninyi ni miti ya bushtani Yangu, lazima maze matunda mema nay a ajabu, ili ninyi wenyewe na wengine mpate kufaidika nayo. Kwa hiyo inampasa kila mmoja kujishughulisha katika ufundi na kazi (mbali mbali), kwa maana humo ndimo ilimo siri ya mali, Enyi watu wenye akili! Kwa maana matokeo hutegemea juu ya njia, na rehema ya Mungu itakuwa ya kutosheleza kabisa kwenu. Miti isiyozaa matunda imekuwa na daima itakuwa kwa ajili ya moto.

81

EWE MTUMISHI WANGU!

Watu duni kabisa kuliko wote ni wale wasiotoa matunda duniani. Watu kama hao kwa kweli wanahesabiwa kama kati ya wafu, hapana, afadhali ya wafu mbele ya Mungu kuliko watu hao wavivu na wasio na thamani.

82

EWE MTUMISHI WANGU!

Watu bora kabisa kuliko wote ni wale amao hupata riziki kwa kazi zao na kutumia juu yao wenyewa na juu ya ndugu zao kwa upendo wa Mungu, Bwana wa dunia zote.

Bibi Arusi asiyeelezeka na waajabu, aliyefichwa kabla ya haya chini ya utaji wa maneno sasa, kwa rehema ya Mungu na fadhili Yake takatifu, amedhihirishwa hata kama nuru ing’aayo inayotawanywa na uzuri wa Mpendwa. Nashuhudia, Enyi marafiki! Kwamba fadhili imekamilika, hoja imetimizwa, hakika imeonekana, na ushahidi umethibitishwa. Acha sasa ionekane ni nini jitihada zenu zitadhihirisha katika njia ya kujitenga. Kwa jinsi hii fadhili takatifu imetolewa kwa utimulifu kwenu na kwa wale walio mbinguni na duniani. Sifa zote ziwe kwa Mungu, Bwana wa Dunia zote.

Bahá'u'lláh

Windows / Mac