Ee Mungu wangu! Huyu ni mtumishi Wako na mwana wa mtumishi Wako ambaye amekuamini Wewe na ishara Zako, na kuelekeza uso wake Kwako, amejitenga kabisa kutoka kwa vyote ila Wewe. Wewe hakika, ndiwe wa wale ambao huonyesha rehema, mwenye rehema kabisa.
Mtendee, Ee Ewe Ambaye husamehe dhambi za watu na kusetiri kasoro zao, kama istahilivyo mbingu ya Baraka Yako na bahari ya rehema Yako. Mjalie kuingia katika mipaka ya rehema Yako bora kabisa ambayo ilikuwapo kabla ya kuanzishwa kwa dunia na mbingu. Hakuna Mungu ila Wewe, Asameheaye daima, Karimu Kabisa.
*Ndiposa tena, arudie mara sita maamkuzi “Alláh’u’Abhá”, na tena arudie mara kumi na tisa kila moja ya aya zifuatazo:
Sisi sote, hakika, twamwabudu Mungu.
Sisi sote, hakika twasujudu mbele ya Mungu.
Sisi sote, hakika tumejitoa kwa Mungu.
Sisi sote, hakika, twamsifu Mungu.
Sisi sote, hakika, twatoa shukrani kwa Mungu.
Sisi sote, hakika, tu wenye subira katika Mungu.
*(Ikiwa marehemu ni mwanamke, hebu aseme: Huyu ni mtumishi Wako wa kike na binti wa mtumishi Wako wa kike, n.k. . . . )
- Bahá'u'lláh
Ee Mungu wangu! Ee Ewe msamehe dhambi, Mpaji thawabu, mwondoa huzuni!
Hakika, nakusihi kusamehe dhambi za wale walioacha vazi la kimwili na wamepaa kwenye ulimwengu wa kiroho.
Ee Bwana wangu! Uwatakase kutokana na makosa, ondoa huzuni zao, na ubadilshe giza lao katika mwanga. Wafanye waingie bustani ya furaha, uwatakase kwa maji safi kabisa, na uwajalie waone utukufu Wako kwenye mlima ulio bora kabisa.
- `Abdu'l-Bahá